Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SektaMaji Mradi wa Usimamizi wa Rasilimali Maji

Tanzania imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi na za aina mbalimbali za maji zikiwemo mito, maziwa, maeneo chepechepe na chemchemi zinazozalisha (rasiliamali za maji jadidifu za juu ya ardhi  za kila mwaka), wa matumizi mbalimbali. Sekta hii inayoongozwa na mkurugenzi mwenye wajibu wa kutathmini kias na ubora na kufuatilia rasilimali za maji. Aidha nashughulika na usalama wa mabwawa. Kutkana na hali hiyo, Kitengo hiki kinakusanya data za matumizi ya majina za kihaidrolijia; kinakusanya na kusimamia data za visima vyote vya maji na kukagua mifumo ya utoaji wa maji iliyopo. Pia na wajibu wa kupanga na kutafiti, kusimamia, kuhimiza sheria na masuala ya mazingira yanahohusiana na rasilimali za maji.

Kitengo hiki pia hutoa msada wa kiufundi kuhusiana na   ujenzi wa visima vya maji na utekelezaji, uhandisi unaohusu maji, udhibiti wa mafuriko na uwanda wa mafuriko. Kitengo kinatoa program mbalmbali za elmu na kuhamasisha matumizi bora ya rasilimali za maji za taifa. Sekta hii inasimamia  shughuli za  Ofisi za Maji ya Mabonde na kuzipatia msaada wa kiufundi.

Zaidi ya hapo inaratibu ushiriki wa Wizara katika mazungumzo ya kitaifa na kimataifa, juhudi na miradi inayohusiana na uendelezaji, usimamizi na matumizi ya rasimali za maji za taifa za mipakani. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya Wizara ya Maji: www.maji.go.tz  

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-12-10 20:01:48
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0