Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SektaSheriaMpango wa Maboresho wa Sekta ya Sheria

Katika kutambua changamoto zinazoikabili sekta ya sheria, Serikali ya Tanzania imedhamiria kutekeleza  marekebisho hayo kwa lengo la kuwahakikishia watu kupata haki kwa kupitia upatikanaji wenye tija wa huduma za msaada wa sheria.  Malengo ya Programu ya marekebisho ya sekta ya sheria (LSRP) katika muktadha huu ni pamoja na:

  • Kasi ya mamlaka ya kutoa haki, uwezo wa kumudu na kupata haki kwa vikundi vyote vya jamii.
  • Kuhamasisha uadilifu na uweledi wa maofisa wa sheria.
  • Kuhakikisha mfumo wa sheria na usimamizi na marekebisho ya kiwango cha juu kabisa kwa mienendo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

URATIBU NA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA PROGRAMU

Ili kutekeleza kwa ufanisi maeneo haya, LSRP imetumia ushirikiano na watoa msaada wa kisheria kama mkakati wake muhimu.  taratibu za ushirikiano kati ya LSRP na LAP zinakusudia kuimarisha upataji wa haki.  Aidha, LSRP imeunda Kamati ya Uendeshaji kwa madhumuni yatakayowezesha AZISE mashirika yanayosaidia sheria kuwa wanachama wanaotenda.  LAP wanaohusika moja kwa moja ni LHRC, NOLA, TAWLA, WLAC,utoaji wa msaada wa sheria wa chuo kikuu huria cha Tanzania (OUTLAC), kamati ya msaada wa sheria ya shule ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

TLS imewezesha uanzishwaji wa mtandao wa watoa huduma ya sheria na pia kupeleka juhudi zake kwenye kurasimisha wasaidizi wa sheria.  TLS imefanya utafiti wa msingi wa wasaidizi wa sheria nchini Tanzania ili kupata taarifa itakayowezesha utoaji wa uamuzi.  Mwaka 2008, Wizara ya Katiba na Sheria iliunda kitengo cha  Huduma za kisheria  kwa Wananchi na ndani ya kitengo hicho ipo sehemu mahususi ya msaada wa kisheria.  Huko  Zanzibar, Wizara ya Katiba na Sheria iko kwenye hatua ya awali ya kuandaa programu kwa ajili ya marekebisho ya sekta ya sheria.  Katika sehemu hii utaona Programu ya marekebisho ya sekta ya sheria ya Tanzania bara.

Mpango wa Maboresho wa Sekta ya Sheria
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-12-03 06:46:46
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0