Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SektaSheriaHuduma ya Huduma za sheria kwa Umma

Wizara ya katiba na sheria imeanzisha Huduma za Sheria kwa Umma (PLSD) yenye kitengo cha msaada wa sheria. Idara iliundwa ili kutengeneza upataji wa haki na kuboresha huduma za msaada wa sheria. Miongoni mwa majukumu makuu ya idara ni pamoja na kuratibu huduma za msaada wa sheria. Ni wajibu wa idara hii kuhakikisha upatikanaji sera na sheria kwa ajili ya kuandaa mfumo unaofaa na unaowezesha wa msaada wa sheria na kazi ya wasardizi wa mawakili nchini Tanzania.

Ili iweze kutekeleza majukumu yake, Idara ya Sheria kwa Umma, iliunda kikosi kazi chenye LAPs za ngazi ya taifa (TAWLA, WLAC,NOLA na LHRC) mashirika haya pia ni wajumbe wa Kamati ya Uendeshaji ya LSRP chini eneo la pili la matokeo muhimu kuhusu huduma za sheria. Eneo hili la matokeo muhimu linaratibiwa na Chama cha Sheria Tanganyika (TLS). Matokeo ya utafiti yamethibitisha kuwa idara ya PLSD inapanga kufanya utafiti na desturi bora za utangazaji kumbukumbu kutoka nchi kama Malawi na Afrika Kusini kwa lengo la kuboresha  huduma za sheria nchini Tanzania na kurudufu desturi bora hizo. Utafioti utakuwa na umuhimu mkubwa na matokeo yatatoa taarifa  ya uamuzi na afua zitakazoboresha mfumo wa sheria kwa ajili ya msaada wa sheria na kazi ya wasaidizi wa sheria nchini Tanzania. Kwa upande mwingine watoa huduma za sheria waliohojiwa wamesema kwamba majukumu na wajibu uliopewa PLSD yangetekelezwa ipasavyo zaidi kama kingekuwa chombo/mamlaka inayojitegemea/huru.  Kwa hali tija kwa ajili ya uratibu wa watoa huduma ya sheria na kuongeza upataji wa haki nchini Tanzania. Sababu zilizotelewa kwa maoni hayo ni pamoja na ukweli kwamba upatikanaji wa msaada wa sheria nchini ni miliki ya sekta za asasi za kiraia, licha ya mchango wa vyombo vya serikali za mitaa kama vile mabaraza ya kata.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-12-02 17:41:30
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0