Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SektaSheriaMahakama za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mahakama za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zimepangwa kwa kufuata muundo rahisi na unaoeleweka wenye mahakama za juu na mahakama ndogo na mahakama maalumu ya katiba, inayoundwa tu patokeapo  mgogoro wa kikatiba kati ya Zanzibar na Tanzania Bara. Katika historia ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika, Mahakama Maalumu ya Katiba haijawahi kuundwa, licha ya kutokubaliana kwa wazi kwenye tafsiri na hali ya muungano. Mahakama za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zimeadhimishwa na katiba, na kwa sheria za manispaa za Zanzibar na Tanzania Bara.

Katika katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sura ya 5, inataja Mahakama kuu Mahakama za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa Tanzania  Bara, Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mahakama ya Rufaa ya Jamuhuri ya Muungano na Mahakama Maalumu ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano. Idara ya mahakama imeelezwa katika Sura ya 5, Ibara za 107A, hadi 113A za Katiba ya Jamuhuri  ya Muungano , kwa ajili ya Idara ya Mahakama ya Tanzaniana Ibara za 114 hadi 115 kwa Idara ya Mahakama ya Zanzibar. Sehemu ya 5 na 6, Ibara za 116 hadi 124 za katiba zinaeleza mahakama ya rufaa (Mahakama ya Juu) ya Tanzania na Sehemu ya 7, Ibara za 125 hadi 128 zinaeleza Mahakama Maalumu ya Katiba. Hii ni mahakama maalumu kuamua masuala yanayohusu mgogoro wowote wa katiba ndani ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mahakama ya Rufaa ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni mahakama ya juu kabisa ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Ibara ya 117 ya Katiba. Mahakama ya Rufaa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni taabisi ya kweli ya muungano kwa sababu ina mamlaka ya kisheria ya nchi kwa rufaa zinazotoka Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar. Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Tanzania ndiye mkuu wa mahakama ya Rufaa na Idara ya Mahakama ya Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar kwa mamlaka ya kukata rufaa. Mahakama ya rufaa imeundwa na Jaji Mkuu na si chini ya majaji wa rufaa wangine wawili, lakini jopo kamili halipungui majaji watano wa rufaa. Hata hivyo, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwa kawaida inakutana kama jopo la majaji watatu wa Rufaa isipokuwa wakati wa chemba ambapo husikilizwa na Jaji mmoja. Sehemu hii inakueleza orodha ya Mahakama Tanz nia Bara.

Mahakama Maalumu ya Katiba Muundo wa Mahakama Tanzania Bara
Mahakama Kuu ya Tanzania Mahakama ya Rufani
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-12-02 11:27:22
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0