Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SektaSheriaVyombo vya Sheria vya Wizara

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa tangazo la kumpa majukumu Waziri (chombo) katika tangazo la serikali Nam. 494, la 17 Desemba, 2010. Kwa mujibu wa Hati hiyo ya kisheria, Rais aliunda Wizara ya Sheria na Katiba iliyopewa mamlaka ya mambo ya katiba  kutunga, kufuatilia na kutathmini, usimamizi wa sheria, sera na usimamizi wa haki za binadamu nchini. Wizara itakuwa na wajibu wa kuratibu na kufuatilia utendaji wa taasisi utakazozipata kwenye sehemu hii zikiwemo Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Marekebisho ya Sheria, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Chuo cha Sheria Tanzania na Wakala ya Usajili, Ufilisi na Udhamini.

Mamlaka ya Wizara ni kuhakikisha kuwepo kwa haki na kusimamia kufanya kazi vizuri kwa mfumo wa sheria nchini unaosaidia  kuwepo kwa amani na utulivu, na hivyo maendeleo ya uchumi wa jamii. Jukumu lake ni kuishauri serikali katika mambo yote ya sera yanayohusu uendelezaji wa sekta imara ya sheria yenye uwezo wa kusimamia wahusika mbalimbali kwa lengo la kuhimiza kuheshimu haki za raia (utawala bora) utulivu wa kisiasa na kiuchumi.  Wizara inaongozwa na Waziri na Katibu Mkuu.

Mahakama Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tume Ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT)
Wakala Wa Usajili, Ufilisi Na Udhamini (RITA) Chuo cha Uendeshaji wa Mahakama, Lushoto
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-12-02 10:40:36
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0